Ticker

6/recent/ticker-posts

RATIBA YA LIGI KUU TZ BARA KESHO

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Apr.12,2016 SAA 11:12 JIONI
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania inatarajiwa kuendelea kesho Jumatano, kwa michezo miwili ya viporo kuchezwa katika
viwanja vya Manungu Turiani mkoani Morogoro na uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Young Africans wanaoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, watakua wenyeji wa Mwadui FC inayokamata nafasi ya sita katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Wakata miwa wa Turiani, Mtibwa Sugar walio katika nafsi ya nne ya msimamo wa ligi kuu watawakaribisha Azam FC walio juu yao nafasi ya tatu, mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Manungu Turiani mkoani Morogoro.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments