Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendeleo mwishoni mwa wiki hii kwa michezo sita itakayofanyika
kwenye viwanja mbalimbali nchini.
Mabingwa wanaotetea taji hilo, Yanga ya Dar es Salaam itakuwa mgeni wa Toto Africa katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa CCM-Kirumba jijini Mwanza huku Coastal Union ikipambana na African Sports kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Mechi nyingine zitakuwa ni kati ya Mwadui FC watakaokuwa wenyeji wa Stand United kwenye Uwanja wa Mwadui, Shinyanga wakati Mbeya City watakuwa wageni wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Manungu, Mvomero mkoani Morogoro na katika Dimba la Sokoine jijiji Mbeya Tanzania Prisons itaumana na JKT Ruvu katika mfululizo wa mechi za ligi hiyo.
Jumapili Simba itaikaribisha Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Michezo Zote zitaanza saa 10.00 jioni na kurushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni ya Azam.

0 Comments