Ticker

6/recent/ticker-posts

ABAJALO,PAMBA FC,MIGHTY ELEPHANT YA SONGEA KUGOMBEA KUPANDA LIGI DARAJA LA KWANZA MSIMU UJAO

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Apr.23,2016 SAA 08:02 MCHANA
Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuanza kwa ligi ndogo Mei 11,
2016 katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam itakayozishirikisha jumla ya timu nne.
Timu zilishoshika nafasi ya pili katika msimamo wa SDL kwa kila kundi, Abajalo FC (Dar es salaam), Pamba FC (Mwanza), Mvuvumwa (Kigoma), Mighty Elephant (Songea) zitacheza ligi hiyo kusaka timu mbili zitakazoungana na timu nne za juu kupanda ligi daraja la kwanza (FDL) msimu ujao.
Klabu nne za Allicane Schools (Mwanza), Mshikamano FC (Dar es salaam), Mbeya Warriors (Mbeya) na Singida United (Singida) zilizoongoza msimamo wa makundi ya SDL zitaungana na timu mbili kupanda ligi daraja la kwanza msimu ujao.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments