Klabu maarufu ya soka ya nchini Uingereza ya Sunderland AFC ambayo inashiriki katika ligi kuu ya nchini Uingereza ijulikanayo
kama Barclays Premier League, leo imetangaza kushirikiana na kampuni ya Acacia Mining plc kuendeleza soka nchini.
kama Barclays Premier League, leo imetangaza kushirikiana na kampuni ya Acacia Mining plc kuendeleza soka nchini.
Sunderland pia imekuwa na uhusiano mzuri na makampuni mengine ya hapa nchini.
Ushirikiano huu ni mkakati wa klabu hiyo kuimarisha uhusiano na taasisi mbalimbali zilizopo barani Afrika na utanufaisha jamii kupitia mpango wa kampuni ya Acacia wa kusaidiajamii, ikiwemo kuendeleza michezo nchini Tanzania.
Kupitia klabu za soka za wilayani Tarime naKahama, klabu ya Sunderland AFC itatenga wiki 10 kwa mwaka kufanya kazi na klabu za wilaya hizi kukuza mpira wa miguu. Ushirikiano huu ni sehemu ya shughuli mbalimbali zinazoendeshwa na Acacia kusaidia jamii kupitia mfuko wa kampuni uitwao Acacia Maendeleo Fund.
Katika kufanikisha mchakato huo Mkuu wa kitengo cha kuendeleza mchezo wa soka kimataifa wa klabu hiyo,ambaye atasimamia shughuli zaushirikiano huu nchini,Graham Robinson tayari ametembelea nakufahamu maeneo amabayo yamelengwa kunufaika na mradi huu.
“Wachezaji wengi wa soka wameanzia kucheza mpira na kukuza vipaji vyao katika ngazi ya vilabu vya jamii. Na sisi kwa ushirikiano wa muda mrefu na taasisi mbalimbali barani Afrika katika kuwekeza kwenye jamii na miradi ya elimu, tumefanikiwa kujijengea sifa kwenye hili. Hivyo basi,kwa kushirikiana na Acacia tutaweza kutimiza malengo ya mradi huu,” alisema Graham Robinson.
Mbali na kushirikia na kampuni ya Acacia, klabuya Sunderland AFC kwa hapa nchini pia ina ushirikiano wa muda mrefu na kampuni ya kuzalisha umeme ya SymbionPower, ambapo kwa kushirikiana kwao walifanikisha ujenzi wa kituo cha Jakaya M Kikwete Youth Park, kilichopo jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake,MkurugenziwaBiashara wa Klabu ya Sunderland,Gray Hutchinson amesema wamefurahishwa na hatua ya klabu hiyo kuzidi kujiimarisha nchini Tanzania kwa kuingia katika ushirikiano na kampuni ya Acacia Mining; “Tumeshirikiana na taasisi kadha wa kadha katika kufanikisha miradi mbalimbali ya kijamii nakuendeleza michezo barani Afrika,hasahasanchini Tanzania. Kwa kuimarisha ushirikiano wetu, tumejijengea mtazamo chanya kibiashara na kijamii hivyo kusambaza ujumbe wa klabu yetu na wakati huohuo kufanya mabadiliko katika jamii,” alisema.
Naye Makamu wa Raisi wa Acacia anayeshughulika na masuala ya shirika,DeoMwanyika alisema “Ushirikiano huu ni mmoja kati ya mingi tuliyonayo, ambayo inalenga kunufaisha jamii hasa zilizozungu ka migodi yetu mitatu hapa nchini.Tunaelewa umuhimu wa kuwapatia watoto elimu ya awali aidha ya darasani au ya uwanjani ilikuendeleza vipaji,hivyo tunaona ushirikano wetu huu ukiwapatia vijana fursa ya kuendeleza vipaji vyao huku wakijifunzakutoka kwa wataalamu waliobobea katika soka.”
Alisema ushirikiano huu utazidi kunoa vipaji vya mchezo wa soka,ambapo Sunderland AFC pia itawapatia makocha ujuzi wa kufundisha soka ambao watavifundisha vilabu vidogo vidogo vilivyopo kwenye jamiina kuleta mabadiliko makubwa katika soka kwa vijana kike na wakiume walioko katika kanda ya ziwa ndani miaka michache ijayo. Vilevile, Sunderland AFC itafanya kazi kwa ukaribu na klabuya Stand United ili kufanikisha mkakati huu ambao umelenga kuwahusisha na kuwanufaisha vijana wa jinsia zote,ambapo pia fursa hii itatumika kuwaelimisha watoto wa kike umuhimu wa kujiendeleza kimasomo.


0 Comments