Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Feb.05,2016 SAA 10:02 JIONI
Ligi Daraja la Kwanza nchini (FDL) raundi ya 13 inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa timu 24 [kucheza michezo 12
katika viwanja tofauti, huku kundi A na C kukiwa na ushindani mkali kwa kila timu kuwania kupanda ligi kuu ya Vodacom msimu ujao.
katika viwanja tofauti, huku kundi A na C kukiwa na ushindani mkali kwa kila timu kuwania kupanda ligi kuu ya Vodacom msimu ujao.
Kundi A, African Lyon watawakaribisha Polisi Dar katika uwanja wa Mabatini – Mlandizi, Ashanti United dhidi ya KMC uwanja wa Karume, huku Jumapili Kiluvya wakiwakaribisha Polisi Dodoma uwanja wa Mabatini – Mlandizi na Friends Rangers wakicheza na Mji Mkuu uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
Kesho Jumamosi, Kundi B Polisi Morogoro watacheza dhidi ya Njombe Mji uwanja wa Jamhuri, Morogoro, Kurugenzi FC dhidi ya JKT Mlale uwanja wa Wambi – Iringa, Burkinafaso dhidi ya Lipuli na Kimondo watawakaribisha Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Vwawa – Mbozi.
Kundi C, Polisi Mara FC watawakaribisha Panone FC uwanja wa Karume mjini Musoma, Geita Gold watacheza dhidi ya JKT Oljoro uwanja wa Nyankumbu mjini Geita, JKT Kanembwa watakua wenyeji wa JKT Oljoro uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, huku Rhino Rangers wakicheza dhidi ya Mbao FC uwanja wa Ali Hassani Mwinyi mjini Tabora.
RATIBA YA SDL RAUNDI YA 7
Raundi ya saba ya Ligi Daraja la Pili nchini (SDL) inaendelea wikiendi hii kwa michezo 12 kuchezwa nchini, kwa timu 24 kusaka pointi kutoka makundi ya A,B,C na D kuwania nafasi nne za juu ili kuweza kupanda ligi daraja la kwanza msimu ujao.
Kundi A, Leo Ijumaa Abajalo Tabora watakua wenyeji wa Mvuvumwa uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora, Green Warriors dhidi ya Singida United uwanja wa Mabatin Mlandizi (jumatatu) na Mirambo FC watacheza dhidi ya Transit Camp siku ya jumatatu uwanja wa Ali Hassani Mwinyi mkoani Tabora.
Kundi B, Kesho Jumamosi AFC ya Arusha watakua wenyeji wa Alliance Schools uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Madini FC watacheza dhidi ya JKT Rwamkoma uwanja wa Mbulu, huku Bulyanhulu FC watawakaribsiha Pamba FC uwanja wa Kamabrage mjini Shinyanga.
Kundi C, Leo Ijumaa Abajalo Dar watacheza dhidi ya Mshikamano uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, kesho Jumamosi Kariakoo FC watawakaribisha Changanyikeni katika uwanja wa Ilulu – Lindi, na Cosmopolitani watacheza dhidi ya Villa Squad siku ya jumatatu katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
Kundi D, Jumamosi Mighty Elephant watacheza dhidi ya Wenda FC uwanja wa Majimaji mjini Songea, Mbeya Warriors watawakaribisha Mkamba Rangers uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, huku Jumapili Sabasaba FC wakicheza dhidi ya African Wanderers uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
0 Comments