Ticker

6/recent/ticker-posts

TAARIFA JUU YA KIFO CHA KIONGOZI WA ZAMANI WA SIMBA,NA KUWASILI KWA RAIS WA AFC TANZANIA

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Jan.18,2016 SAA 11:33 JIONI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Asia (AFC) na Makamu wa Rais wa FIFA, Sheikh Salman Bin Ebrahim Al
Khalifa amewasili nchini leo mchana na kupokelewa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi.
Sheikh Salman amekuja nchini kwa matembezi ya siku ya mbili na atakua na mwenyeji wake Rais wa TFF, Jamal Malinzi.
Kesho Jumanne, Sheikh Salman Bin Ebrahim Ali Khalifa atamtembelea ofisini Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel.

TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI SIMBA SC

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetuma salamu za rambirambi kwa klabu ya Simba SC, kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo miaka ya 1998-2000 Seleman Said ‘Yeltisn’ kilichotokea jana jijini Dar es salaam.
Katika salamu hizo TFF imesikitishwa na kifo cha kiongozi huyo, ambaye alingoza klabu ya Simba SC na kupelekea kupewa jina la utani la ‘Yelstin” kutokana na ufanisi wake katika kazi na misimamo akifananishwa na aliyekua Rais wa kwanza Urusi wakati huo Boris Yeltsin.
TFF kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini inawapa pole familia ya Seleman Said ‘Yelstin’ ndugu jamaa, marafiki, uongozi na wanachama wa klabu ya Simba kufuatia kifo hicho, na kusema wako pamoja katika kipindi hiki cha maombelezo.
Mazishi ya marehemu Selaman Said ‘Yelstin’ yanafanyika leo saa 10 kamili jioni katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) 

Post a Comment

0 Comments