Ticker

6/recent/ticker-posts

TRA NA TFF SAKATA LAO LIMEFIKIA HAPA...(AUDIO)

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Des.08,2015 SAA 02:05 USIKU

Shirikisho la soka nchini TFF,limesema kuwa bado linawasiliana na mamlaka ya mapato Tanzania TRA,ili kuweza kupata suruhisho
mara baada ya mamlaka hiyo kuzuia fedha katika akaunti zote za shirikisho hilo.

 Mamlaka ya Kodi ya Mapato (TRA) mkoa wa Ilala, ilizuia fedha kwenye akaunti zote za Shirikisho hilo kwa madai ya kulipwa kiasi cha Shilingi 1,637,334,000 (bilioni 1.6 tshs) ikiwa ni kodi kwa kipindi cha 2010 – 2013 sehemu kubwa ikiwa ni makato kwenye mishahara (PAYE) ya walimu wa kigeni, Jan Poulsen, Kim Poulsen na Jacob Michelsen na vilevile kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye mchezo wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) dhidi ya Brazili uliofanyika mwaka 2010.

Afisa habari wa TFF, Baraka Kizuguto ameelezea juu ya taarifa iliyotolewa wiki iliyopita,kuhusu sakata hilo.

BONYEZA PLAY KUSIKILIZA
U15 YAREJEA DAR


Ziara ya timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15) iliyoanzia kanda ya ziwa na kanda ya Magharibi kisha kuendelea katika nchi za Rwanda, Uganda na Kenya mwezi huu imesitishwa kutokana na kufungwa akaunti za Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA).
Timu hiyo ya vijana iliondoka wiki iliyopita kuelekea jijin Mwanza, ambapo iliagwa na kukabidhiwa bendera ya Taifa na katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel, ilicheza mchezo mmoja wa kirafiki na timu ya Alliance kabla ya kuelekea mkoani Kigoma.
Ikiwa Kigoma U-15 ilicheza michezo miwili ya kirafiki na timu ya kombaini ya mkoa wa Kigoma U-15, jumapili ikacheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya Burundi U-17, na jana asubuhi kuanza safari ya kurejea jijini Dar essalaam.
Awali ziara ya timu hiyo ya U-15 ilikua iendelee katika mji wa Kigali kwa kucheza na U17 ya Rwanda, Kampala kucheza na Uganda U17, jijini Nairobi kwa kucheza na U17 ya Kenya na kumaliza ziara hiyo kwa kuchez ana U15 kombaini ya mkoa wa Arusha Disemba 23, na kurejea jijin Dar es salaam Disemba 24, 2015.

U-15 inajiandaa na michuano ya Viajana U17 kuwania kufuzu kwa Mataifa ya Afrika mwaka 2017 nchini Madagascar itakayoanza kutimua vumbi Juni 2016.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) 

Post a Comment

0 Comments