Kocha Mourinho yuko katika wakati mgumu baada ya kupoteza michezo tisa kati ya 16 ya Ligi kuu.
Wenger, ambaye timu yake ya Arsenal iko katika nafasi ya pili na ikitafuta alama mbili tu ili kuweza kuongoza ligi inayoshikiliwa na Leicester.
"Kama unaniuliza, malengo, ikiwa Chelsea itakuwa inapigana kwenda chini,mimi nasema: hawana nafasi," alisema Wenger.
"Watakuwa na wakati mgumu lakini siyo katika vita ya kushuka daraja ".
"Lakini sitaki kufanya tathmini na mambo mengine yoyote zaidi kwa Chelsea. Tatizo langu si kwao, tatizo langu ni mchezo dhidi ya Manchester City siku ya Jumatatu usiku."
Wenger awali alisema yeye ana huruma kwa mameneja wote wanapokuwa wanakabiliwa na wakati mgumu, na alipoulizwa kama yeye alishiriki kutokuwa sawa kwa Mourinho, Mfaransa huyo alisema: "Angalia, nilishatoa jibu."
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)
0 Comments