Jumla ya waamuzi chipukizi 29 wasiokua na beji za FIFA kutoka nchi 28 barani Afrika wanatarajiwa kuhudhuria kozi ya
waamuzi inayoandaliwa na FIFA kwa kushirikiana na CAF itakayofanyika kuanzia kesho Jumamosi tarehe 26 –30 Septemba mwaka huu jijini Dra es salaam.
Kozi hiyo itaendeshwa na wakufunzi kutoka katika nchi za Afrika Kusini, Malawi, Misri na Mauritius itafanyika katika hoteli ya Holiday Inn iliyopo jijini Dar es salaam ambapo waamuzi chipukizi kutoka Tanzania watakohudhuria ni Abdallah Kambuzi (Shinyanga) na Shomari Lawi (Kigoma).
Lengo la kozi hiyo ni kuwaanda waamuzi wanaochipukia ili baadae kuweza kuwa waamuzi wa FIFA ambao watatumika kwa michuano mbalimbali.
MALINZI ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI
Rais wa Shrikisho la Mpira wa Migu nchini (TFF), Jamal Malinzi ametuma salam za rambirambi kwa Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry kufuatia vifo vya mahujaji zaidi ya 700 vilivyotokea Maka wakati wa kuhiji.
Katika salam zake kwenda kwa mufti mkuu, Malinzi amewapa pole waislam wote duniani kufuatia vifo vya mahujaji hao zaidi ya 700 vilivyotokea juzi na majeruhi zaidi ya 400 wakati wa ibada ya hija.
Malinzi amesema kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini TFF inawapa pole wafiwa wote, ndugu jamaa na marafiki na kuwatakia majeruhi afya njema na kusema ipo pamoja nao katika kipindi hichi kigumu cha maombelezo.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments