![]() |
| Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Klabu ya Yanga Jerry Muro na kocha mkuu wa klabu ya Yanga Hans Van Pluijm |
Wakati mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara Dar es salaam Young Afrika ikitarajia kucheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi kuu Tanzania Bara
Dhidi ya Coastal Union hapo kesho katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam,Hii leo uongozi wa klabu hiyo yenye makao yake makuu katikati ya makutano ya Twiga na Jangwani jijini Dar es salaam, umeneno na waandishi wa habari juu ya mikakati yao.
Dhidi ya Coastal Union hapo kesho katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam,Hii leo uongozi wa klabu hiyo yenye makao yake makuu katikati ya makutano ya Twiga na Jangwani jijini Dar es salaam, umeneno na waandishi wa habari juu ya mikakati yao.
Uongizi wa klabu ya Yanga umesema kila kitu kimekamilika kuelekea msimu mpya wa Ligi wa ligi kuu Tanzania Bara 2015/2016 na wamejipanga kwa ajili ya kutetea Ubingwa wao.
Akizungumza na Waandishi wa Habari ,Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Klabu ya Yanga Jerry Muro amesema wamejipanga kuanza Ligi vizuri na kuahakikisha wanafanya vizuri katika michezo ya Mwanzoni.
Jerry Muro amesema kwa maandalizi yao ya kabla ya Msimu,watahakikisha wanautetea ubingwa wao wa Ligi kuu ya Tanzania Bara.
Jerry Muro Pia amesema Yanga Tayari imelipa kiasi cha shilingi Milioni 1 na Laki 1 kwa shirikisho la Soka nchini Tanzania Tff kwa ajili ya Leseni za wachezaji wa timu A na timu B,pia imelipa kwa shilikisho hilo Dola elfu 2 kwa ajili ya wachezaji wao wa nje ya nchi katika harakati za usajili.
Taarifa zilizo zagaaa katika mitandao zilisema kuwa Yanga walikataa kuwalipia wachezaji wao ada ya dola za Kimarekani 2,000 (TSh. Milioni 4) kila mmoja hivyo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) liliwazuia,lakini Yanga imekana madai hayo.
Yanga imewataka mashabiki wa klabu hiyo kutoa wasiwasi kuwa huenda wachezaji wao wa kimataifa wasicheza katika mchezo wao wa kesho na Coastal na kuwataka mashabiki hao kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuishangilia Timu hiyo.
![]() |
| kocha mkuu wa klabu ya Yanga Hans Van Pluijm |
Wakati huo huo kocha mkuu wa klabu ya Yanga Hans Van Pluijm amesema hapendi kuzungumza Sana kwani mpira hauchezwi mdomoni, bali unachezwa kwanye uwanja,lakini kikosi chake kiko vizuri kwa ajili ya Msimu mpya na kuelekea mchezo wa kesho, na kusema Juma Abduli atakosa mchezo huo kwa sababu alipata kadi nyekundu katika mchezo wao wa mwisho wa Ligi msimu uliopita.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .



0 Comments