Ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa 2015-16, kesho inaingia katika mzunguuko wa tano kwa kushuhudia michezo
saba ikichezwa katika viwanja tofauti.
saba ikichezwa katika viwanja tofauti.
1.Mkoani Morogoro, mabingwa watetezi Dar es salaam young Africans watakua wakihitaji kuendeleza wimbi la ushindi mbele ya Mtibwa Sugar ambao wameanza vyema msimu huu kwa kushinda michezo yao yote.
Kwa upande wa wenyeji wa mchezo wa kesho huko mkoani Morogoro, wakata miwa ambao maskani yao makuu ni huko Manungu, Tuariani Mtibwa Suagar utamsikia Afisa habari wa Mtibwa Sugar Tobias Kifaru akijinasibu juu ya mchezo huo.
2.Kwenye uwanja wa Azam Complex jijini Dar es salaam, Costal Union watakuwa wageni wa Azam FC ambao msimu huu wameanza vyema mikiki mikiki ya ligi kuu ya kushinda michezo yao minne iliyiopita.
Kuelekea katika mchezo wa kesho afisa habari wa Azam FC Jaffary Iddy ametoa neno na kuwataja majeruhi wa timu yao.
3.Kwa upande wa Costal Union kupitia kwa afisa habari wao Oscar Assenga amesemaje juu ya hali ya kuokota point moja moja katika michezo miwili na kufungwa miwili?
4.Mjini Songea mkoani Ruvuma, Wanalizombe Majimaji wao kesho watakuwa na kibarua cha kuwakabili Ndanda FC kutoka mkoani Mtwara ambao wamefunga safari kutoka mkoani Tanga ambapo walikubali kufungwa na Africans Sports bao moja kwa sifuri.
Kocha msaidizi wa Majimaji FC Hassan banyai amezungumza na kipindi hiki na kueleza hali ya kikosi chao kuelekea katika mchezo huo wa kesho ambao amekiri utakua mgumu.
KIMATAIFA
Utasikia Ratiba za mechi za ligi ya mabingwa Ulaya September 29
SIKILIZA HAPO CHINI
0 Comments