Ticker

6/recent/ticker-posts

WAKONGWE WA TAIFA STARS KUANZA KESHO KATIKA MECHI YA AZAM NA YANGA TAIFA

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.AUG.21,2015 SAA 09:34 MCHANA
Mchezo wa Ngao ya Jamii kuashiria kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu ya Vodacom nchini (VPL) utachezwa kesho
jumamosi katika uwanja wa Taifasaa 10 kamili jioni, ambapo utazikutanisha timu za Azam FC dhidi ya Yanga zote kutoka jijini Dar es salaam.
Tiketi za mchezo huo zitaanza kuuzwa kesho asubuhi katika magari maalum maeneo ya uwanja wa Taifa, ambapo kiingilio cha chini kitakua shilingi elfu saba (7,000) na kiingilio cha juu ni shilingi elfu thelathini (30000) kwa VIP A.
Kuelekea mchezo huo maandalizi yote yamekamilika, ulinzi na usalama utakuwepo wa kutosha, wapenzi na wadau wa mpira wanaombwa kujitokeza kushuhudia mchezo huo. Vimininika, silaha au vitu vinavyoweza kuhatarisha usalama havitaruhusiwa kuingia uwanjani.
Kabla ya mchezo kati ya Azam FC dhidi ya Yanga SC kutakua na mchezo wa utangulizi utakaozikutanisha timu ya wachezaji wa zamani wa timu ya Taifa (Taifa Stars Legends) dhidi ya Ukonga Veterani.
Milango ya uwanja wa Taifa itakua wazi kuanzia majira ya saa 5 kamilia asubuhi kutoka nafasi kwa wapenzi wa mpira kuweza kuingia uwanjani mapema.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments