Ticker

6/recent/ticker-posts

TAARIFA RASMI KUHUSU UCHAGUZI WA TEFA,NA KOZI YA MAKOCHA LESENI ‘C’

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.AUG.19,2015 SAA 10:33 JIONI
Wa kwanza ofisa habari wa DRFA Omary Katanga katikati ni Rashid Sadall Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya DRFA,kuli ni katibu wa kamati ya Uchaguzi Fahad Kayuya
Kamati ya uchaguzi DRFA inaelekeza kamati ya uchaguzi ya TEFA kufanya uchaguzi wa viongozi,jumapili tarehe 23/08/2015 katika
ukumbi wa JKT kama ilivyopangwa kufanyika hapo awali.
Kamati pia inapenda  kuutarifu umma kuwa mchakato huu una Baraka zote kutoka TFF,hivyo uingiliaji wowote unakwenda kinyume na ibara ya 6(1)ya kanuni za uchaguzi za TFF 2013 na ibara za 52(6) na 56(6)(a) za katiba ya TFF ambazo zinaelekeza kuwa majukumu ya uchaguzi yapo chini ya kamati ya uchaguzi.
Itakumbukwa uchaguzi huo uliokuwa ufanyike jumapili ya tarehe 16,08,2015 uliahirishwa na kamati ya uchaguzi ya Tefa licha ya shirikisho la TFF kuagiza ufanyike,na hivyo mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi DRFA wakili Rashid Saadallah akaitaka kamati hiyo ya TEFA kumuandikia barua kueleza sababu ya kuahirisha uchaguzi huo.
baada ya kupitia sababu hizo,ndipo DRFA ikatoa majibu kwa kuelekeza uchaguzi huo sasa kufanyika jumapili hii.
KOZI YA MAKOCHA LESENI ‘C’ ILIYOANDALIWA NA  DRFA SASA YAIVA,WADAU WAOMBWA KULIPIA  ADA ZAO  MAPEMA.
kozi ya ukocha leseni C inatarajiwa kufanyika kuanza tarehe 28. 08. 2015,katika ukumbi wa TFF Uwanja wa Karume, ambapo washiriki wanakumbushwa kulipia ada zao za ushiriki ambayo ni shilingi  TZS 250,000.

Katika kzoi hiyo inategemewa kuwepo na madarasa mawili ya wanafunzi 30 kila darasa.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) . 

Post a Comment

0 Comments