Ticker

6/recent/ticker-posts

KARUMA MWENYEKITI MPYA TWFA

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.AUG.29,2015 SAA 04:20 USIKU
Uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu nchini (TWFA)  umemalizika ambapo Amina Karuma amechaguliwa kuwa
mwenyekiti mpya wa chama hicho, kufuatia uchaguzi uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Nafasi ya katibu msaidizi imekwenda kwa mwandishi wa habari za michezo Someo Ng’itu, na nafasi ya wajumbe wa kamati ya utendaji ya TFWA imekwenda kwa Debora Mkemwa na Theresia Mng’ongo.
Mgeni rasmi katika uchaguzo huo alikuwa ni katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine ambapo na uchaguzi ulisimamiwa na Kamati ya Uchaguzi ya TWFA chini ya uangalizi wa Jeremia Wambura kutoka kamati ya Uchaguzi ya TFF.
TFF inawapongeza viongozi wapya waliochaguliwa na kuwatakia kila la kheri katika majukumu hayo mapya, na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika maendeleo ya mpira wa miguu ya wanawake nchini.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) . 

Post a Comment

0 Comments