Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Jun 23,2015 SAA 09:38 USIKU
Bingwa wa Wimbledon mwaka  2013 Andy Murray ataingia katika mashindano wiki ijayo  katika wakati mzuri baada ya kuchukua rekodi
kwa kushinda mataji manne katika mashindano ya AEGON.
Lakini pia Bingwa mtetezi wa Wimbledon Novak Djokovic anajinasibu kurejesha taji lake  hilo.
Lakini mchezaji mwingine wa Tennis Greg Rusedski ambaye yeye alishawahi kufika robo fainali ya Wimbledon, mwaka 1997,anasisitiza Andy Murray anaweza kushindana taji hilo mwaka huu na kuwa No 1 kwa Dunia .
Greg Rusedski anaamini Andy Murray  yuko katika ubora mzuri ' na anaweza kujinyakulia taji la pili la Wimbledon mwaka huu. 
Rusedski, alifika robo fainali ya Wimbledon, mwaka 1997
"Bado nadhani anaweza kushinda taji la pili - ame kuwa akivutia sana," Rusedski aliiambia Sky Sports .
"Novak Djokovic ni wazi ni bingwa mtetezi, lakini ataendelea kuwa katika sura kuu. Nadhani alicheza vizuri hapa.alishinda kwa mara ya nne,ana amafanikio yake ya mwaka 2009, 2011, 2013 na sasa ni mwaka 2015.
"Nadhani Andy Murray tangu afunge ndoa, kwa vile alianza na Jonas Bjorkman na Amelie Mauresmo, kila kitu kitakwenda kutokana nguvu ileile."
Rusedsk ana matumaini kwamba sare nzuri itamuweka Djokovic katika upande mwingine dhidi ya Murray wakikutana fainali,
"Nadhani kwa Murray, kama ataweza kukutana na Djokovic katika fainali, basi pengine inaweza kuwa bingwa wa Wimbledon tena".alifafanua Greg Rusedski 

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)