Ticker

6/recent/ticker-posts

KOCHA MKUU WA SIMBA NA KOCHA WA MAKIPA WAWASILI

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Jun 26,2015 SAA 12:57 JIONI

Kocha mkuu wa timu ya Simba Dylan Kerr na kocha wa makipa Abdul Iddi Salim wamewasili mchana huu jijini Dar es
Salaam tayari kuanza kazi ya kuinoa timu ya Simba.

Kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere walilakiwa na wajumbe wa kamati ya utendaji Collin Frisch na Said Tulliy.

Akizungumza na mara baada ya kuwasili. Kocha Kerr alipata wasaa wa kuzungumza na simbasports.co.tz na kusema “nafurahi sana kufika Tanzania na kupata mapokezi makubwa ambayo sikutegemea. Kwa sasa nina hamu ya kukutana na timu na uongozi wa Simba baada ya hapo ndipo nitakuwa na la kusema”. Kocha Kerr alisema “amefanya utafiti na kupata dondoo za mpira wa Tanzania hata wapinzani wetu nimewasikia”

Kocha Kerr pia ana uzoefu wa kufundisha na kufanya kazi Afrika, ameshawahi kufanya kazi na kufundisha timu za South Africa NFD Nathi Lions FC na  South Africa Thanda Royal Zulu FC kutoka Afrika Kusini

Kerr ana leseni ya daraja A na B ya ukocha aliyotunukiwa na Shirikisho la soka la Ulaya (UEFA) huku pia akiwa na uzoefu wa utawala katika fani ya michezo.

Klabu ya Simba inafuraha kubwa kuingia mkataba na kocha huyu mwenye uzoefu na weledi wa kutosha, tunaamini atakuwa chachu ya mafanikio pia kunoa vipaji vya wachezaji wa Simba.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)

Post a Comment

0 Comments