Azam FC imewaruhusu wachezaji wake watatu waliomaliza mikataba yao kutafuta timu nyingine.
Wachezaji hao ni Gaudence Mwaikimba, Amri Kiemba (mkopo toka Simba) na Wandwi Jackson.
Pia klabu imerefusha mikataba ya wachezaji waliokuwa wakikaribia kumaliza mikataba yao. Wachezaji hao ni Said Morad, Erasto Nyoni, Dedier Kavumbagu, Khamis Mcha, Waziri Salum, Brison Raphael, Joseph Kimwaga, Mudathir Yahya na Farid Mussa.
Hadi sasa Klabu haijaingia mkataba na mchezaji yoyote toka nje.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)

0 Comments