Mashindano ya Klabu Bingwa kata ya kawe
yameanza kutimua vumbi siku ya jumamosi may 2 mwaka huu Katika Viwaja vya
Tanganyika Pekaz ,kata ya Kawe,Kinondoni jijini Dar
Mashindano hayo
yana Lengo la kuinua vipaji
katika kata ya Kawa
yanashirikisha timu Nane zinazocheza katika mfumo wa
Nyumbani na Ugenini.
| Gabliel Munasa akizindua mashindano ya Klabu Bingwa kata ya Kawe |
Akizindua
mashindano hayo Ndugu Gabliel Munasa ambaye
pia ni mkazi wa Kawe,amesema ,kupitia
michezo vijana wanaweza kupata ajira,huku kupitia mashindano hayo wakiwa
wamejiwekea malengo ya kuweza kupata vijana wakakamavu na wachapakazi katika Kata ya Kawe,kwani kata hiyo imekuwa ni mfano wa kuigwa katika
maswala ya michezo.
Aidha Gabliel Munasa ameongeza kuwa, anatambua umuhimu wa
mashindano hayo, na ndio maana wakati
akiwa Nchini Marekani siku tatu zilizopita
alipopokea mualiko wa kufungua mashindano hayo,ameweza kufika haraka kwa ajili ya Shughuli hiyo
kwa kuwa jamii ya wana Kawe imeweza kumpa nafasi hiyo.
Pia Gabliel Munasa amesema zawadi katika mashindano hayo,mshindi
wa kwanza atapata Jezi seti mbili na mpira Mmoja pamoja na Laki tano,Mshindi wa
pili atapata Jezi seti mbili na mpira mmoja.
WITO KATIKA MASHINDANO HAYO NI:VIJANA KUJIANDIKISHA KATIKA
DAFTARI LA KUPIGIA KURA ,ILI KUWEZA KUMCHAGUA KIONGOZI WANAYEMTAKA KATIKA MWAKA HUU WA
UCHAGUZI.
Timu zinazo shiriki katika mashindano hayo ni Market,Mji mpya,G4c,Bodaboda
Gsf,Champion,Halisi,Shelaton pamoja na Black Star
ANGALIA PICHA ZA UZINDUZI
| Kushoto:Gabliel Munasa akikabidhi Jezi |
| Kulia:Gabliel Munasa akitoa vifaa kwa timu zinazishiriki mashindano hayo |
| Market wakipambana na Mji mpya |
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

0 Comments