Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers amefurahia timu yake kutoka katika wakati mgumu wa mwanzo wa msimu ,na sasa
ameanza kufikiria mikakati ya kukaa juu, katika nafasi ya kwanza ya msimamo wa ligi kuu ya England.
ameanza kufikiria mikakati ya kukaa juu, katika nafasi ya kwanza ya msimamo wa ligi kuu ya England.
| Liverpool ilishinda 2 - 1 dhidi ya Manchester City |
Baada ya msimu wao wa mwanzo wa mapambano, Liverpool sasa kwa upande wao katika Ligi Kuu wako katika nafasi ya tano - pointi mbili nyuma Manchester United walioko katika nafasi ya nne.
Rodgers alisema:.. "Inachukua muda kidogo kupanda na kukaa katika njia fulani ya kucheza,....lakini tumekaa imara, wakati wa sasa ni mgumu, Tumepata ufumbuzi na sisi tunacheza katika kiwango cha juu".
"Ni vigumu.lakini kukaa katika nafasi nne za juu daima imekuwa ndio lengo letu. Tunataka kupata nafasi hii mwishoni mwa msimu".
"Kila mchezo kuna ushindani mkubwa na kila timu ni bora.tunakwenda katika kila mchezo na kuheshimu mpinzani ila na amini tunaweza kushinda."
Baada ya ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Burnley mwezi Desemba, Rodgers anatarajia mtihani mwingine mgumu kutokana kwa timu hiyo,mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Anfield siku ya kesho Jumatano usiku.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments