SIKIA HII,Utafanya nini endapo utapewa taarifa kuwa umetimuliwa kazini?.
Taarifa kutoka Sky Sports News HQ siku ya Jumapili jioni,zilisema kwamba Pearson alikuwa amepoteza kazi yake na klabu hiyo ya Ligi Kuu, kabla ya klabu hiyo kutoa taarifa yake rasmi ikisisitiza kuwa kocha huyo atasalia katika klabu hiyo.
Lakini vyanzo vya Sky vimeeleza kwamba Pearson na wafanyakazi wake walikuwa wafukuzwe na mmoja wa wamiliki wa klabu hiyo, na kumchukuwa kocha mwingine masaa matatu baadaye.
Suala hilo kuu lilizua mjadala katika mkutano na vyombo vya habari siku ya jana Jumatatu alipokuwa akizungumzia mchezo wa Leicester City dhidi ya Arsenal utakaopigwa hii leo Jumanne usiku,na ingawa Pearson alikuwa na nia ya kuzungumzia mchezo wao utakaopigwa katika dimba la Emirates, waandishi wa habari wakambana kwa kumtaka azungumzie uvumi huo juu ya mustakabali wake, naye akasema kwamba hakuna uhakika juu ripoti za awali kwamba alikuwa atimuliwe,na akisisitiza kuwa ni uongo na uvumi tu unaozungumzwa.
Meneja wa Leicester City Nigel Pearson |
"Sijawahi kuzungumza sana kuhusu mahusiano ya ndani katika klabu,daima nimekuwa daima na kazi nzuri na uhusiano na bodi.," Alisema Pearson.
"Wakati mwingine Kuna uvumi - kwa bahati mbaya, wakati mwingine habari zinavuja. Lakini mimi bado nina wajibu wa kuwaongoza wachezaji.Nisingependa kutoa taarifa nje , lakini mimi nitaendelea kuwepo".
"Naelewa mnataka nini, maswali, lakini nina imani kwa watu mimi nina fanya kazi, wafanyakazi wangu na wachezaji ambao ni muhimu zaidi kwangu kuliko kushughulika na taarifa ambazo zina misingi ya uvumi tu."
Alipoulizwa kama amepewa uhakika juu ya mustakabali wake na klabu hiyo, alisema: "Nimefanya mazungumzo (na bodi) na kama nitakuwa na kitu cha kusema, itabidi niseme nao kwa namna sahihi kwa watu sahihi".
"Tuna mchezo kesho na mtazamo wangu na wachezaji ni kuona juu ya nini tunaweza kufanya kesho usiku." alisema Meneja wa Leicester City Nigel Pearson
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments