Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.Aug.05,2014 SAA 08:00 Alasiri
Siku mbili baada ya uongozi wa klabu ya Simba kuwafuta uanachama wanachama 72 kwa mujibu wa katiba ya Simba akiwemo Michael Richard Wambura,hatimaye wambura
ameibuka na kupinga maamuzi hayo kwa kusema wao Bado ni wanachama halali wa klabu hiyo.
ameibuka na kupinga maamuzi hayo kwa kusema wao Bado ni wanachama halali wa klabu hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari hii Leo Michael Wambura amesema kuwa, kufukuza wanachama si kutatua matatizo ya klabu hiyo bali ni kwenda kinyume na katiba na kumfanya mwanachama aliyefukuzwa kwenda mahakamani kwani ndio sehemu ya mwisho ya kupata suruhisho kwa mujibu wa katiba ya nchi ya Tanzania.
Wambura amesema Bado kuna mkanganyiko wa Katiba yaTanzania inayoruhusu kwenda mahakamani kutafuta suruhisho na ile ya simba inayokataza kwenda mahakamani.lakini ameapa kuwatetea wanachama hao,kwani kukaa kimya itakuwa ni dhambi na usaliti kwa kuwaacha wanachama hao.
Pia Wambura amesema swala lake la kufukuzwa uanachama amelipeleka kwa wanasheria wake,ili kujua kipi halali na si halali, na Siku chache zijazo atatoa tamko lake.lakini amesema bado hajapata barua ya maamuzi hayo ya mkutano wa Simba.
0 Comments