Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers anasisitiza kumsaini Mario Balotelli si chaguo baya na pia amekiri kuwa timu yake
ina haja ya kufanya maboresho baada ya wao kupachikwa mabo 3-1 na Manchester City.
Mabao mawili ya Stevan Jovetic na bao moja la Sergio Aguero yaliipa ushindi City licha ya bao la kujiunga la Pablo Zabaleta.
Livepool walikuwa na wakati mgumu katika Monday Night Football dhidi ya City,licha ya kuanza vizuri katika mchezo wao ufunguzi mwishoni mwa wiki, ambao waliibuka na ushindi dhidi ya Southampton, na kudhani kuwa ndani ya Etihad wataweza kufanya vile vile.
habari ya kuwasili kwa Balotelli inatoa matumaini kwa Livepool na Rodgers anaamini, licha ya tabia yake ya zamani, mchezaji huyo wa Italia anaweza kufanya vizuri zaidi katika uwanja wa Anfield.
"Maisha yangu yote, nawapa wachezaji nafasi,"
"(Balotelli) ana umri wa miaka 24, na imekuwa ni baba sasa"
" anajua wajibu wake, si tu kwa ajili yake mwenyewe lakini na kwa ajili ya klabu hii kubwa".
"tutamuelekeza,hakuna kutofautiana , Mario Balotelli ni sehemu ya timu yetu".alisema Brendan Rodgers
Akitafakari juu ya mchezo wa Ligi Kuu waliofungwa katika uwanja wa Etihad, Rodgers anaona msimu huu City bado watakuwa na ushindani mkubwa, pamoja na Liverpool katika kinyang'anyiro cha kugombea taji.
ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments