Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.Aug.02,2014 SAA 06:48 USIKU
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ana mipango ya kufanya usajili zaidi msimu huu, lakini amekubali kwamba nahodha
Thomas Vermaelen anaweza kuondoka Emirates.
Wenger tayari ametumia zaidi ya £ 60m kwa kumsaini Mathieu Debuchy, Alexis Sanchez, David Ospina na Calum Chambers na Mfaransa huyo ana ujasiri wa kufanya usajili zaidi kwa kikosi chake.
" bado niko wazi kufanya mengi zaidi na hebu usisahau ndiyo kwanza Agosti mosi leo na dirisha la uhamisho linafunga siku ya kwanza ya Septemba," alisema.
"Kila mtu inavuta pumzi kwa sasa kwa sababu kila mtu anaangalia katika michezo ya maandalizi kuona yupi ambaye bado wanamuhitaji.
"Watu wamesajili sehemu kubwa ya watu wanaowahitaji na sehemu ya mwisho itafanyika baada ya michezo ya maandalizi kuona nini amekosa."
Alipoulizwa kama anatarajia kumbakisha Vermaelen katika klabu msimu ujao, Wenger alisema: "Kwa sasa, yuko hapa".
"Na anaweza kuondoka. Ndiyo, inawezekana kwamba huenda akaondokana, na kama akiondoka tutakuwa na mbadala wake kwa sababu yeye ni mchezaji muhimu katika kikosi chetu".
"Natarajia akae lakini bila shaka hakucheza michezo ya kutosha mwaka jana. Kwangu mimi yeye ni mchezaji muhimu sana lakini sikuweza kumpa michezo mingi mwaka jana hivyo nitaona."
Wenger pia aliulizwa siku ya Ijumaa na waandishi wa habari kuhusu uvumi juu ya kumuhitaji mchezaji wa Porto raia wa Colombia kiungo Juan Quintero, lakini bosi huyo wa Gunners kinamna alikanusha kuwa mambo hayo yalipangwa, na akasisitiza kuwa hana majadiliano yoyote ya kumuhitaji mshambuliaji wa AC Milan na Italia Mario Balotelli .
ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments