Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.JUL.28,2014 SAA 8:40 USIKU
Kutokuwa na uwezo kwa Manchester United wa kutoweza kumiliki mchezo kumemfanya kocha wao mpya Louis van
Gaal kukasirika licha ya kushinda 3-2 dhidi ya Roma siku ya Jumamosi usiku nchini Marekani.
Rooney alifunga katika dakika za 36 na 44 kwa penalti, wakati bao lingine la United lilifungwa na Juan Mata dakika ya 39.
Mabao ya Roma yalifungwa Miralem Pjanic dakika ya 75 na mkongwe Francesco Totti kwa penalti dakika ya 88 katika mchezo huo.
Rooney akishangilia na wenzake, Antonio Valencia na Ander Herrera baada ya kufunga bao la kwanza |
Juan Mata alifunga bao kipindi cha kwanza |
Ni ushindi wa pili mfululizo wa Louis van Gaal baada ya ule wa mabao 7-0 dhidi ya LA Galaxy wiki iliyopita tangu kuchukua hatamu Old Trafford na kuona timu yake ikiendeleza ubabe kwenye ziara yao ya Marekani .
"Nafurahi kwamba tumekuwa washindi akini utendaji haukuwa mzuri," kocha huyo mwenye umri wa miaka 62 aliiambia tovuti ya klabu. "Zaidi ya watu 54,000 walikuja kutuangalia sisi lakini tunaweza kufanya vizuri zaidi".alisema
"Hatuwezi kutumia hali ya hewa hii ya moto. Nadhani sisi hatukucheza mechi vizuri kwa sababu ya urefu wa uwanja, hewa, kwa sababu ya hayo yote wachezaji wangu walishindwa" aliongezea
ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments