Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.JUL.17,2014 SAA 04:10 USIKU
Louis van Gaal amesema Manchester United ni klabu kubwa duniani lakini anataka kuijenga upya baada ya kufanya
vibaya msimu uliopita.
Van Gaal amefanya mkutano wake wa kwanza na vyombo vya habari tangu achukue uongozi Old Trafford baada ya kuiongoza Uholanzi kushika nafasi ya tatu katika Kombe la Dunia.
Mholanzi huyo huyo amesema United ni klabu yenye nguvu dunia lakini pia aliwakumbusha mashabiki kuwa maboresho makubwa yanahitajika msimu huu.
"'Msimu uliopita mlikuwa wa saba hivyo hii si klabu kubwa,mnajithibitishia wenyewe, "alisema.
"Lakini duniani kote watu wanazungumza juu ya Manchester United - hiyo ndiyo tofauti".
"Ni changamoto kubwa na kwa sababu hiyo ndiyo iliyonifanya nichague klabu hii".
"nimewahi kufundisha Barcelona, Ajax na Bayern Munich ambao wote ni No 1 katika nchi zao. Sasa mimi niko Manchester United ambayo ni No 1nchini Uingereza".
"Sijawahi kufanya kazi katika Ligi Kuu ya England, na hiyo ndio changamoto kubwa".
"Wakati nikiwa Barcelona ilikuwa ligi bora. Wakati nikiwa Germany ilikuwa ligi bora".
'Sasa niko hapa labda hii ni ligi bora.'
Aliendelea: "Wakati kuna changamoto kama hii siwezi kwenda likizo. Hii pia ni likizo kwangu kwa sababu mimi napenda kazi. "
Back in the day: Van Gaal says he has talked to Sir Alex Ferguson, here showing him Barcelona's ground
Class of 92: Van Gaal confirmed there will be roles on his staff for United legends Phil Neville and Paul ScholesBut we need to be careful because you cannot over-train players.'
Van Gaal alikataa kuzungumzia wachezaji atakao wasajili , lakini anataka kukipa kikosi chake nafasi ya kumvutia kabla ya msimu.
Pia amebaini kwamba Luka Shaw na Ander Herrera walisajiliwa kwa kibali chake.
ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments