Uongozi wa klabu ya Yanga umemtambulisha rasma kwa waandishi wa habari Kocha mbrazil Marcio Marcel Maximo kama ndio
kocha atakayeweza kukinoa kikosi cha timu hiyo katika msimu ujao wa Ligi kuu Tanzania Bara.
kocha atakayeweza kukinoa kikosi cha timu hiyo katika msimu ujao wa Ligi kuu Tanzania Bara.
Utambulishwaji huo ulifanywa katika makao makuu ya Klabu hiyo jijini Dar es salaam na kuuzuliwa na waandishi wa habari wengi pamoja na wanachama waliokuwa nje kwa ajili ya kumshuhudia kocha huyo.
Wakala aliyefahamika kwa jina moja la Ally ndiye aliyeweza kufanikisha mipango hiyo ya kumleta maximo.
Marcio Maximo |
Leonardo Neiva |
"nawashukuru wana Yanga kwa uvumilivu wao kwani kwa miaka mitatu sasa nawasiliana na Marcio Maximo " aliseama Ally na kuongeza kuwa mtazamo wa kocha huyo ni kuinua vipaji na kuwataka wana Yanga wavumilie na kumpa muda kwa ajili ya kupata mafanikio.
Maximo amesaini mkataba wa miaka miwili ya kuifundisha Yanga na amekuja na msaidizi wake Leonardo Neiva.
Naye Maximo amesema kuwa sio rahisi kuipandisha timu ya Yanga na kupata mafanikio makubwa bali kwa kushirikiana kila kitu kitafanikiwa.
Kutoka kushoto:Wakala Ally,Marcio Maximo na Leonardo Neiva |
Waandishi wa habari waliojitokeza katika mkutano |
"Wakati nakuja kwa mara ya kwanza nilikuwa nasikia Yanga na Simba,lakini niliporejea tena kwa mara ya pili sasa nasikia Azam, mbeya City na virabu vingine" alisema kocha huyo huku akikubali kuwa upinzani ni mkubwa.
Kocha Marcio Maximo anaaza kazi rasmi Siku ya Jumatatu na na atakuwa na msaidizi wake Leonardo Neiva ambapo watajihusisha sana na Vijana pamoja na timu ya wakubwa.
USISAHAU KULIKE PAGE YA FACEBOOK ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI, BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)
0 Comments