Mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez amesimamishwa shughuli zote za soka kwa muda wa miezi minne kwa
kumng'ata mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini.
Kamati huru ya Fifa ya kinidhamu imempiga marufuku baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kupatwa na hatia ya utovu wa nidhamu.
Suarez pia imefungiwa kucheza mechi tisa ya kimataifa, na kutolewa nje katika mashindano ya Kombe la Dunia nchini Brazili pamoja na kutozwa faini ya dola elfu mia moja.
Tukio kumng'ata mchezaji mwenzake lilitokea siku ya Jumanne katika mchezo wa kombe la dunia wa kundi D, ambapo Uruguay ilifuzu hatua ya mwisho 16.
USISAHAU KULIKE PAGE YA FACEBOOK ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI, BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)
0 Comments