Ticker

6/recent/ticker-posts

TP MAZEMBE WALALA BAO 1 KWA O DHIDI YA EL HILAL MBELE YA SAMATA NA ULIMWENGU

Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.May. 16,2014 SAA 05:00 USIKU
Muda mchache uliopita TP Mazembe ya Jamhuri ya Kodemokrasia ya Kongo katika mchezo wao wa
kwanza hatua ya makundi katika Ligi ya Mabingwa Afrika,mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Khartoum nchini Sudan,,timu hiyo imeanza vibaya baada ya kufungwa bao 1-0 na El Hilal Omduran .

Bao la El Hilal Omduran lilifungwa na Salah Al Jizoli dakika ya 51 katika mchezo huo wa kundi A,ambapo mtanzania Mbwana Samatta alianza na Thomas Ulimwengu akitokea benchi dakika ya 66 kwenda kuchukua nafasi ya Rainford Kalaba.

Samata na Ulimwengu watawasili nchini Jumamosi saa 7.30 mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines wakitokea Khartoum, Sudan,kwa ajili ya mechi ya Kombe la Afrika dhidi ya Zimbabwe (Mighty Warriors) itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments