Ticker

6/recent/ticker-posts

(PICHA)TAZAMA WENGER ALIVYOOGESHWA BILA KUPENDA NA VIJANA WAKE BAADA YA KUTWAA KOMBE LA FA

Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.May. 17,2014 SAA 04:49 USIKU
Arsene Wenger
Arsenal hii leo wameweza kuwapa raha mashabiki wao waliosubili kwa muda wa miaka 9 bila taji lolote, baada ya hii
leo kufanikiwa kunyakuwa Kombe la FA katika msimu huu wa 2013-2014  kwa kuinyuka Hull City mabao 3 kwa 2.
Going nowhere: Arsenal boss Arsene Wenger has confirmed he will be staying on as manager
Going nowhere: Arsenal boss Arsene Wenger has confirmed he will be staying on as manager
Shower time: Lukas Podolski of pours beer over Wenger after their FA Cup win
Shower time: Lukas Podolski of pours beer over Wenger after their FA Cup win

Arsene Wenger
Baada ya ushindi huo wachezaji wa timu hiyo walishindwa kujizuia kutokana na furaha waliokuwa nayo,na kujikuta wakimwagia bia kocha wao Arsene Wenger na kisha kumrusha rusha juu kama furaha yao kwa kutwaa taji hilo la FA.
Arsenal
Katika mchezo Washika bunduki hao walianza kwa kusuasua baada ya City kupata mabao mawili ya mapema kabisa dakika ya 4 kupitia kwa James Chester   na Curtis Davies  dakika ya 9 ya mchezo huo,lakini wakazinduka baada ya Santi Cazorla kupachika bao la kwanza kwa Arsenal dakika ya 17 na kwenda mapumziko Hall City wakiwa wanaongoza kwa mabao mawili kwa moja.

Katika kipindi cha pili Arsenal walifanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika ya 71 kupitia kwa Laurent Koscielny na timu hizo kumaliza dakika 90  wakiwa wamefungana mabao 2 kwa 2.
Mchezo ukaamuliwa kuongezwa dakika za ziada na hatimaye vijana waArsene Wenger  wakachomoka na na ushindi kwa bao la tatu lililofungwa na Aaron Ramsey,dakika ya 109 ya muda wa ziada.

Post a Comment

0 Comments