Rio Ferdinand wa Manchester United mustakabari wake umefika kikomo katika klabu hiyo, baada ya beki huyo
mkongwe kupewa taarifa kwamba klabu haitaweza kumuongezea tena mkataba mpya.
Inafahamika kwamba mkuu wa Old Trafford Ed Woodward alitoa taarifa za Ferdinand mwenye miaka 35 katika chumba cha kubadilishi nguo siku ya Jumapili katika mchezo mwisho dhidi ya Southampton.
Watu kadhaa ambao walikuwepo wakati akielezea taarifa hizo walishtushwa na uamuzi wa Woodward kwa beki hiyo aliyekaa kwa miaka 12 na klabu ya United.
Mlinzi huyo wa zamani wa England aliwaambia wachezaji wenzake kwamba sare ya bao 1-1 katika uwanja wa St Mary ni mchezo wake wa mwisho kwa klabu hiyo na aliwataka kutia saini mpira kama zawadi ya kumbukumbu.
Ferdinand, ambaye alikuwa mchezaji ghali zaidi katika historia ya mpira wa Uiingereza alipojiunga na United kutoka Leeds kwa £29.1million mwezi Julai 2002, ametokea katika mechi 455 za United lakini ilikuwa pembezoni chini ya utawala wa David Moyes.
Wakati wa mabadiliko: Louis van Gaal atathibitishwa kama meneja mpya wa United wiki hii |
Msemaji wa Ferdinand alisema: "Rio anakusudia kuendelea kucheza mpira wa miguu".
Mchezaji huyo wa zamani wa West Ham ana ofa za kucheza soka kutoka Ligi Kuu ya Soka ya Amerika, China na Mashariki ya Kati, na huenda akachagua wapi kwa kwenda zaidi ya wiki ijayo.
Katika taarifa yake Ferdinand alisema: "najisikia vizuri na afya tele, niko tayari kwa changamoto mpya na kuangalia mbele kwa chochote kwa ajili ya maisha yangu ya baadaye".
Aliwashukuru wachezaji wenzake, klabu na mashabiki, na kuongeza kuwa 'baada ya miaka 12 ya kucheza vizuri katika klabu bora duniani, nimeamua wakati muafaka kwangu kusonga mbele".
0 Comments