Ticker

6/recent/ticker-posts

MBEYA CITY YAFANYA KWELI KATIKA MCHEZO WAO WA KWANZA,WAIBAMIZA TIMU KUTOKA BURUNDI MABAO 3 KWA 2

Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.May. 24,2014 SAA 01:55 USIKU
Mbeya City imefanikiwa kuchomoka na ushindi wa mabao 3
kwa 2 katika mashindano ya  Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) yanayoitwa Nile Basin,ambapo wawakirishi hao wa Tanzania bara walikuwa wakicheza na timu ya Academie Tchite ya Burundi.

Mabao ya Mbeya City yamefungwa na Paul Nongo dakika 15, mshambuliaji mpya Themi Felix kutoka Kagera Sugar dakika ya 27,na Mwagane Yeya dakika ya 37.

Katika mechi nyingine wenyehi Al-Merreikh wameichapa 3-0 Polisi ya Zanzibar na Victoria University ya Uganda ikaibamiza 1-0 Malakia ya Sudan Kusini, wenyeji wengine, Al-Shandi waliichachafya kwa mabao 2-1 Dkhill ya Djibouti.

Post a Comment

0 Comments