Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.May. 16,2014 SAA 10:55 JIONI
Lionel Messi imekubali mkataba mpya na klabu ya Barcelona ambao utafanya kuwa mchezaji anayelipwa kiwango
kikubwa duniani.
Maelezo ya mkataba mpya hayakowazi, lakini mkataba huo umefuatia majadiliano ya muda mrefu.
Imeripotiwa kuwa mchezaji huyo mwenye miaka 26 alisisitiza juu ya kumpita mchezaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo katika kiwango cha kulipwa kama mchezaji duniani.
Ripoti kutoka Hispania zimesema mkataba mpya wa Messi utamfanya nyota huyo wa Argentina kulipwa mshahara wa £16.3m kwa mwaka,pamoja na motisha ya kufanya vizuri katika michezo.
Taarifa ya Tovuti rasmi ya klabu ilisema: "FC Barcelona imefikia makubaliano ya kurekebisha masharti ya kisheria katika mkataba wa Leo Messi na klabu, kama mchezaji bora katika kikosi cha kwanza".
"Mapitio na marekebisho ya mkataba mpya yatasainiwa siku chache zijazo."
Habari za kuongeza mkataba Mpya na kabla ya Barcelona kwa Messi zinakuja siku chache kabla ya timu hiyo kukutana na Atletico Madrid siku ya Jumamosi, ambapo timu ya Barcelona ni lazima ishinde katika mchezo huo ili wawe mabingwa wa La Liga, lakini sare itakuwa nzuri vya kutosha kwa timu Atletico ili nao waweze kushinda La Liga.

0 Comments