Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.May. 16,2014 SAA 02:49 USIKU
David Moyes aliyefukuzwa kazi kama meneja wa magwiji wa ligi ya Premier, Machester United, atafidiwa mamilioni
ambayo hayatazidi herufi moja, mwenyekiti msaidizi mtendaji, Ed Woodward, alitangaza siku ya Alhamisi.
Akihutubia mkutano wa kujadili matokeo ya fedha ya klabu hiyo mwaka huu, Woodward pia aliwaeleza wawekezaji kuwa taaarifa kuhusu mrithi wa Moyes litatolewa ‘hivi karibuni’.
Kocha wa sasa wa Uholanzi, Louis van Gaal, ndiye anayetarajiwa kupewa wathifa huo huku vyombo vya habari vya Uingereza vikitangaza uteuzi wake utafanywa wiki ijayo.
Moyes alipigwa kalamu baada ya kutawala miezi 10 alipojiuzulu kutoka Everton ili kusaini kandarasi ya miaka sita na United kama mrithi wa Sir Alex Ferguson aliyehudumu kwa muda mrefu kabla ya kustaafu mwisho wa musimu jana.
Alitangaza fidia ya Moyes kwa kukatiza mkataba wake itatatuliwa Septemba.
Ijapokuwa United walidorora kwenye uwanja, waliweza kushuhudia ongezeko la asilimia 26 ya mapato yaliyofikia Pauni milioni 115.5 kwa robo ya tatu ya mwaka.
Mapato yaliongezeka kutokana kwa kupanda kwa fedha kutoka ada ya kupeperusha mechi za Premier katika runinga na makubaliano na wafadhili.
Chini ya uongozi wa meneja wa muda, Ryan Giggs, United walimaliza katika nafasi ya saba kwenye Premier na kukosa kufuzu Ligi ya Uropa msimu ujao.
Woodward alisema kukosa kufuzu kuwania kombe kuu la ligi ya mabingwa kutaigharimu klabu hiyo “kati ya pauni milioni 30 za Uingereza” huku akieleza “majuto mengi” kwa United kumaliza katika nafasi ya saba.
Aliapa kuwa miamba hao ambao wametawala Uingereza kwa karne mbili zilizopita wataekeza nguvu kusajili viungo maahiri katika soko lijalo la uhamisho ili kuimarisha juhudi za kurejea kwenye kilele la taifa hilo.
0 Comments