Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.May. 30,2014 SAA 06:01 USIKU
Shirikisho la soka nchini Cameroon na serikali zimekubaliana
kwa pamoja kumlipa kila mchezaji Dola laki moja na elfu nne wakati wa michuano ya kombe la dunia nchini Brazil mwezi ujao.
Fedha hizo zitalipwa kwa wachezaji wa kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 wakati wa michuano hiyo.
Hili suala la mshahara kwa wachezaji wa Cameroon limekuwa tata katika siku za hivi karibuni na hatua hii inaangiziwa kuwa litasaidia kumaliza mzozo huu ambao umekuwa ukiendelea kwa muda mrefu.
Kikosi hicho kikiongozwa na nahodha Samuel Eto'o kilikuwa kimetishia kugoma kuanzia siku ya Ijumaa ikiwa marupurupu yao yangewekwa wazi na shirikisho hilo la soka.
Mashabiki wa soka nchini humo wamekuwa wakishinikiza kikosi cha Cameroon kuiletea sifa nchi hiyo katika michuano ya Kimataifa kama ilivyokuwa miaka ya 80 na 90 wakati wachezaji kama Roger Milla wakicheza.
Mwaka 2010 Cameroon ilikuwa nchi ya kwanza kubanduliwa nje ya michuano ya kombe la dunia iliyofanyika nchini Afrika Kusini.
0 Comments