Ticker

6/recent/ticker-posts

AKILIMALI AFUNGUKA LEO,ASEMA KUNA NJAMA ZA KUIFANYA YANGA IONEKANE MAGUMASHI

Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.May. 17,2014 SAA 11:50 JIONI
Akilimali (katikati) na baadhi ya wazee wa klabu ya yanga wakizungumza hii leo
Baraza la wazee wa klabu ya Yanga  Leo wametoa wito kwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kuweza kuwapa majibu
haraka juu ya  ombi la klabu hiyo kupewa nafasi ya nyongeza katika eneo la uwanja wao ili kuweza kujenga.

Akizungumza na waandishi wa habari hii leo katibu baraza la wazee Ibrahim Akilimali amesema wamemuandikia barua mkuu wa mkoa wa dar es salaam,lakini  mpaka sasa hawajapata majibu yakuhusiana na ujenzi huo 

"Baraza la wazee na jopo lote,siku ya tarehe 19 tutaenda katika ofisi ya mkuu wa mkua kupata jibu ili tarehe 1 ambayo tutafanya mkutano mkuu wa maandalizi ya uchaguzi tupate cha kusema"

Aidha Mzee Akilimali ameongeza kuwa nia ya kujenga uwanja wanayo,kwani mpaka sasa makampuni mbalimbali yameshapewa tenda.

"Kibali kikitolewa baada ya miezi 6 tutaanza kujenga na ndani ya miaka 2 uwanja utakuwa umekamilika"

Pia wazee wa klabu hiyo wana imini mkuu wa mkoa yuko vizuru,ila tatizo liko kwa madiwani,na kusema kuwa kuna njama za makusudi ili kuizolotesha yanga ionekane magumashi.

Mzee Akilimali alimaliza kwa kusema kuwa,wanataka waambiwe tu kama watapewa au hawatapewa kibali,ili wajue la kufanya,kwani sasa klabu hiyo inataka maendeleo.






Post a Comment

0 Comments