Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA March. 03,2014 SAA 07:32 USIKU
Barcelona imejisogeza nafasi ya pili katika msimamo wa La Liga baada ya Lionel Messi kushuhudiwa kuisaidia timu yake katika
ushindi wa 4-1 dhidi ya Almeria
katika uwanja wa Nou Camp.
MuArgentina huyo alipiga bao lake katika dakika ya 24 na kufanya timu yake iwe inaongoza kwa mabao 2-0 mbele, baada ya Alexis Sanchez kuweza kufunga katika dakika ya 9.
Angel
Trujillo aliweka nyavuni bao moja kwa timu yake iliyokuwa ugenini kwa kichwa katika dakika ya 27 .
Lakini mabao la Carles Puyol dakika ya 83 na Xavi dakika ya 89 yaliwahakikishia pointi 3 muhimu vijana hao wa Gerard Martino.
0 Comments