Ticker

6/recent/ticker-posts

LIGI YA MABINGWA:ALICHOKISEMA JOHN TERRY KUHUSU DIDIER DROGBA BAADA YA MCHEZO WAO

Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA March. 19,2014 SAA 11:16 ALFAJIRI
Nahodha wa Chelsea John Terry anaamini kwamba Didier Drogba
bado yuko katika kiwango cha juu duniani  baada ya kukabiliana na  mshambuliaji huyo katika ambao walishindi mabao 2-0 dhidi ya Galatasaray  usiku wa kuamkia hii leo.

Drogba alikuwa na ufanisi wa juu katika mchezo huo licha ya kushindwa-  na nafasi zikawaangukia Chelsea baada Samuel Eto'o kupachika bao la kwanza mapema tu katika dakika ya 4 na Gary Cahill kupata bao lingine dakika ya 42 na kufanya jumla ya mabao iwe 3-1 na kuifanya Chelsea kutinga katika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya .

Mshambuliaji wa Ivory Coast ambaye alipachika jumla ya mabao 157 katika miaka yake minane akiichezea na The Blues kabla ya kuondoka mwaka 2012 baada ya kufunga penalti ya ushindi katika mchezo wake wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa akiwa hapo, ingawa Jose Mourinho hivi karibuni amefufu uvumi wa kumtaka Drogba kujiunga na klabu hiyo. 
  
Drogba  amepokelewa kishujaa kwa kurudi kwake Stamford Bridge na Terry,Mchezaji mwenzake wa zamani, hakuweza kusema sana juu ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 baada ya kutumia muda wa miaka nane ya pamoja katika timu hiyo. 

"Ana nguvu kwa kweli - hata katika mechi ya kwanza, alikuwa na nguvu hivyo hivyo," aliiambia Sky Sports.
 
"Ikiwa mpira uko mikononi mwa kipa ,hatakama unanguvu, huwezi  kuuchukuwa, sidhani kama kuna mtu yeyote bora katika dunia,ambaye leo amefanya hilo".
 
"Yeye bado ni tishio kubwa na bado yuko juu, mchezaji wa hali ya juu na nadhani ni bora kwangu mimi  na hatimaye ameweza kuonyesha usahihi kwa  mashabiki wa Chelsea usiku wa leo"

"Didi  katika vyumba vya kubadilishia nguo ilikuwa anasema 'hello' kwa kila mtu, ni kama mchezaji wa zamani ameungana tena usiku wa leo lakini ameshinda vizuri, kuna baadhi walikuwa nyuso za furaha na sasa sisi tunazingatia mwishoni mwa wiki."
 
Ulikuwa ni Ushinda wa moja kwa moja kwa Chelsea ambao sasa wanasubiri siku ya Ijumaa katika droo ya  robo fainali na Terry anafurahishwa na timu yake kwa kiwango walichokionyesha .
.
 

Post a Comment

0 Comments