Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA March. 04,2014 SAA 08:43 USIKU
Kocha mkuu wa Nigeria Stephen Keshi ameelezea wasiwasi wake juu Victor Muses baada ya hivi karibuni kutotumika sana katika michezo ya Barclays Ligi Kuu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 ameonekana katika michezo mitano tu akiwa na kikosi cha Liverpool katika mwaka 2014, ikiwa ni pamoja na mchezo mmoja alioanza dhidi ya Bournemouth katika Kombe la FA mwezi Januari.
Keshi hakuweza kuficha wasiwasi wake juu ya mchezaji huyo wa zamani wa Crystal Palace ambaye anaona kama mchezaji muhimu katika mipango yake kwa majira ya Kombe la Dunia nchini Brazil.
Alisema John Obi Mikel hivi karibuni jukumu lake katika klabu ya Chelsea si la kutisha ikilinganishwa na Muses.
Meneja huyo wa Nigeria mwenye umri wa miaka 52 amebaini kuwa atafanya
mazungumzo na Muses wakati akifika Marekani kwa ajili ya mechi ya kirafiki
ya kimataifa wiki hii dhidi ya Mexico katika uwanja wa Georgia Dome huko
Atlanta.
"Sina
tatizo sana na Mikel (hucheza kama mchezaji kinda) kwa sababu yeye ni
mtaalamu. Anapata michezo kwa wakati hapa na pale ambayo ni sawa kwangu mimi.
Lakini Victor (Muses) mimi huwa na wasiwasi kwa sababu
yeye hacheza wakati wote,sina furaha kuhusu hali hii lakini
siwezi kufanya kitu chochote kuhusu hilo.. Mimi najua (meneja wa Liverpool)
Rodgers (Brendan) anataka kushinda kila mchezo na anachagua timu
bora .Lakini mimi itabidi kuzungumza na Victor wakati atakapokuja
Atlanta, "Keshi aliiambia Brila FM katika mahojiano na redio.
Muses amejitokeza katika michezo 15 akiwa na Liverpool msimu huu na amefunga mara
moja katika sare ya mabao 2-2 dhidi ya Swansea Septemba 2013.

0 Comments