Na.Boniface Wambura,IMEWEKWA FEB. 12,2014 SAA 10:06 JIONI
Mechi
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Mbeya City na Mtibwa Sugar iliyochezwa
Februari 9 mwaka huu Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya imeingiza sh.
25,602,000.
Watazamaji
8,534 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyomalizika kwa wenyeji Mbeya
City kuibuka na ushindi wa mabao 2-1. Kiingilio katika mechi hiyo kilikuwa sh.
3,000.
Mgawanyo
wa mapato ulikuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 3,905,389.83, gharama
za kuchapa tiketi sh. 489,500 wakati kila klabu ilipata sh. 6,256,097.05.
Uwanja
sh. 3,181,066.52, gharama za mechi sh. 1,908,639.91, Bodi ya Ligi sh. 1,908,639.91,
Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 954,319.96 na Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA) sh. 742,248.86.

0 Comments