Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA FEB. 1,2014 SAA 02:43 USIKU
Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania imeingia raundi ya 16 hii leo kwa mechi kadhaa kupigwa,ambapo leo (Februari 1 mwaka huu) Simba ilikuwa
mwenyeji wa
Oljoro JKT katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Na katika mchezo huo Simba wakachomoka na ushindi wa nguvu wa mabao 4 kwa 0,na kuifanya timu hiyo itimize alama 30 ikiwa imecheza michezo 15,mabao ya Simba yalifungwa na Jonas Mkude katika dakika ya 19 na mabao mengine matatu ya simba yalifungwa na Amisi Tambwe katika dakika ya 24,29 na 52(HAT TRICK).
Uwanja
wa Azam uliopo Mbagala ulikuwa na mechi kati ya wenyeji Ashanti
United na Mgambo Shooting kutoka Handeni mkoani Tanga,na katika mchezo huo timu ya Mgambo Shootong imechomoka na ushindi wa mabao 2 kwa 0.
Jumapili
(Februari 2 mwaka huu) ni Yanga vs Mbeya City (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam,
saa 10 kamili jioni), na Azam vs Kagera Sugar (Uwanja wa Azam Complex, Chamazi
saa 10 kamili jioni).
Ligi
hiyo itaendelea Jumatano (Februari 5 mwaka huu) kwa mechi kati ya Tanzania
Prisons vs Coastal Union (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Mgambo Shooting vs Ruvu
Shooting (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Rhino Rangers vs Oljoro JKT (Uwanja wa
Ali Hassan Mwinyi, Tabora), na JKT Ruvu vs Ashanti United (Uwanja wa Azam
Complex, Chamazi).

0 Comments