IMEWEKWA FEB. 7,2014 SAA 08:16 USIKU
Mkuu wa majeshi ya Kenya ameviambia vyombo vya habari
kuwa shirika la Ujasusi la Marekani FBI lilikabidhiwa miili ya magaidi
walioshambulia jengo la Westgate nchini Kenya mwaka jana.
Karangi, ameyasema hayoalipokuwa akikitoa
maelezo katika mkutano ulioandaliwa nchini Kenya na baraza la vyombo vya
habari kuhusu ambavyo shambulizi hilo lilishughulikiwa.
Alisema kuwa majeshi yake hatimaye
yaliweza kuwaua magaidi hao, siku mbili baada ya kuvamia Westgate tarehe
21 mwezi Septemba 2013.
Magaidi hao walifyatua risasi kiholela na kuwaua takriban watu 67 huku mamia ya wengine wakijeruhiwa.
Bwana Karangi aliongeza kwamba baada ya shambulizi kuanza Jumamosi magaidi waliuawa siku iliyofuata.
''Miili ya magaidi hao ilikabidhiwa majasusi wa FBI,'' alisema Karangi ingawa hakutoa maelezo zaidi.
Washambuliaji wote wanne walikuwa wenye asili ya kisomali ingawa mmoja kati yao alikuwa ameishi zaidi nchini Norway
Maafisa wa usalama wakati huo wakipambana na
magaidi hao walikuwa wametoa taarifa kuwa Westgate ilivamiwa na
ilivamiwa na magaidi 12 ingawa idadi yao baadaye ilisemekana kuwa
magaidi wanne pekee
Wanamgambo wa Somalia Al- Shabaab walidai
kutekeleza mashambulizi hayo wakisema kuwa ilikuwa onyo kwa serikali ya
Kenya kukoma kujihusisha na vita nchini Somalia ambako wanasadia majeshi
ya Muungano wa Afrika kupambana dhidi ya Al Shabaab.
CHANZO:BBC SWAHILI

0 Comments