Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA JANU. 26,2014 SAA 08:15 USIKU
Raundi
ya 14 ya ligi kuu Tanzania bara imeendelea leo siku ya Jumapili (Januari 26 mwaka huu) kwa mechi
mbili zilizopingwa
katika viwanja viwili tofauti.
katika viwanja viwili tofauti.
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ulikuwa shuhuda wa mechi kati ya
Simba na Rhino Rangers kutoka Tabora,ambapo katika mchezo huo Simba wameibuka na ushindi wa bao 1 kwa 0.
Bao pekee la simba lilifungwa na Ramadhani Singano ‘Messi’ katika dakika ya 13,na kuifanya Simba SC itimize pointi 28 baada ya kucheza mechi 14,
ikiwa imebaki nafasi ya nne nyuma ya Yanga yenye pointi 31, Azam na Mbeya City
pointi 30 kila moja.
| Mashabiki wa simba wanalivyokuwa wanaonekana kwa mbali |
| Kikundi cha kuhamasisha cha Simba |
| Mashabiki wa Simba wanavyoonekana kwa karibu |
Mchezo mwingine ulikuwa ni kati ya maafande wa JKT Ruvu na
Mgambo Shooting waliopambana katika Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam,na timu ya JKT Ruvu ikaibuka na ushindi wa mabao 3 kwa 2 dhidi ya timu ya Mgambo Shooting.
| Simba Sc. wakiomba na kishukuru baada ya amchezo kumalizika |
| Simba haoo,wakiondoka uwanjani baada ya ushindi wa bao 1kwa 0 |
0 Comments