Mhariri:Herman Kihwili.IMEWEKWA DESEMBA 16.2013 SAA 12:09 ASUBUHI
Andre
Villas-Boas alistahili kupewa nafasi ya zaidi ya kuendelea kufanya kazi na
kikosi chaTottenham Hotspur, Harry Redknapp
alisema baada ya mrithi wake huyo kufutwa kazi kama meneja wa klabu hiyo.
Klabu ya Tottenham Hotspur ambayo imemfungia virago kocha wake Andre Villas-Boas
Jumatatu kufuatia kichapo cha mabao 5-0 dhidi ya Liverpool katika
uwanja wa White Hart Lane siku ya Jumapili,kwa sababu ya kukatishwa tamaa katika msimamo wa Ligi Kuu.
Spurs
waliwahi pia kupata kipigo cha mbwa mwizi cha mabao 6-0 kutoka kwa timu ya Manchester City wiki tatu zilizopita na kupata mateso mengine ya aibu ya kufungwa kwa mabao 3-0 na West Ham United mwezi
Oktoba lakini Redknapp anaona ni mapema mno kumuhukumu kijana huyo wa Kireno.
"Nadhani wamechukuwa maamuzi ya haraka sana," aliiambia Radio ya Talksport siku ya Jumatatu. "wanapoteza ushirikiano wa michezo sasa na wako matatani".
"wanafikiri kila mtu ni mzuri katika kazi zao au sio,kama unamchagua mtu
unapaswa kumpa wakati na umuache kufanya kazi," aliongeza Redknapp,
ambaye sasa anafundisha timu ya Queens Park Rangers iliyoshuka daraja lakini wanaongoza katika Championship .
"Ni
mapema mno kuanza kutafuta mtu wa kuziba nafasi yake,ningeweza
kumpa muda na kuona nini anaweza kufanya," alisema kabla ya kutangazwa kuwa Villas-Boas alikuwa amefukuzwa kazi.
Juande Ramos |
Tottenham Hotspur watafunga safari ndefu kuelekea Ukraine kwa ajili ya kukutana na bosi
wa zamani wa klabu hiyo Juande Ramos ambaye sasa anafundisha timu ya Dnipro
Dnipropetrovsk watakapokutana katika mchuano wa Europa League tarehe 20 mwezi wa pili 2014.
Ramos
alikuwa msimamizi wa klabu hiyo ya London kaskazini hapo zamani,alifanikiwa kuongoza kama kocha na klabu ya Tottenham Hotspur jumla ya michezo 54,alishinda michezo 21,alitoka sare michezo 16,akafungwa michezo 17,lakini hakuweza kuwasaidia Tottenham Hotspur kushinda 2008 katika Kombe la Ligi
klabu ya kuondoka katika klabu hiyo.
0 Comments