Ticker

6/recent/ticker-posts

BREAKING NEWS:WANACHAMA WA SIMBA WASEMA WATAMSOMEA ALBADILI MWENYEKITI WAO ISMAIL ADEN RAGE

Mhariri:Herman Kihwili.IMEWEKWA DESEMBA 16.2013 SAA 12:09 JIONI
Wanachama wa klabu ya Simba katika tawi la mpira pesa wameandaa mipango ya kwenda nyumbani kwa Mwenyekiti wa
klabu hiyo Mh.Ismail Aden Rage (MB) mara baada ya mechi ya mtani jembe siku ya jumamosi.
Baadhi ya wanachama wa Simba wakijadiliana katika tawi la mpira pesa
Akizungumza na Jamii na Michezo mmoja wa wanachama wa tawi hilo Hustadh Masud,amesema kuwa hatua ya mwisho watakayoichukuwa wao kama wanachama ni kwamba, siku hiyo ya mechi ya mtani jembe,wakifungwa au wakishinda,watatoka uwamjani moja kwa moja kwa ajili ya kwenda nyumbani kwa Rage na hata wakimkuta mke wa Rage,wataongea naye kwani hata mkewe Rage maswala ya Simba anahusika nayo,kwani wanachama hao wamepata taarifa kupitia katika kamati ya utendaji kuwa pesa za usajili,Rage amekuwa akimpa mkewe kupitia katika akaunti yake.
Hustadh Masud
"Sisi tutafika pale kwa mkewe,tutamwambia kuwa amwambie mumewe ajiuzulu,atuachie simba yetu,tutakaa pale hata kwa siku tatu au siku nne,tutalala na tutaamka,tunamtaka ajiuzulu kwa sababu hatutaki tukafika sehemu ukatokea umwagaji wa damu kwa mambo ambayo yanaepukika"alisema Hustadh Masud.
 
"Inawezekana hii ikawa ndio suruhisho na tutahakikisha hata huyo mkewe asitoke nje,kwani sisi tumeacha majumba yetu kwa hiyo tutakuwa nje na yeye humo ndani asitoke mpaka mume wake atakapotoa tamko la kujiuzulu,na sio kujiuzulu pekeyake vilevile na kutuambia pesa ya kumuuza okwi ziko wapi,lazima sisi kama simba tupae haki yetu,hatulalamikii Okwi kwenda Yanga bali tunalalamikia haki yetu"alifafanua tena.

Aidha Hustadh Masud ameongeza kuwa,kwa kuwa Rage anamshirikisha mkewe,katika swala hili watakwenda nyumbani kwake na hata kama mkewe hajui kuongea kiswahili na kuongea kisomali,watamtafuta msomali ili awatafsilie

"Haiwezekani Rage pesa za Okwi akawa hajapata,kwani hata kwa akili ya mtoto iyo pesa amesha lipwa,hata hivyo waarabu hawana tabia ya kuzurumu kwani ni watu wa dini sana.Sisi tunasema kuwa iyo pesa imesha toka na Rage ameichukuwa isipokuwa anatafuta nafasi ya kuizurumu klabu ya Simba,na hii klabu ni mali yetu sisi wanachama,na sisi kama wanachama tutakwenda kokote kule,na tukishindwa kabisa tutamsomea albadili"alimalizia kusema Hustadh Masud

Post a Comment

0 Comments