Na.Ngonise Kahise,IMEWEKWA NOVEMBA 15.2013 SAA 01:32 USIKU
Mtandao wa wanafunzi nchini(TSNP ) na Jumuiya ya
kutetea haki za binadamu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDHRA), wamemtaka
Waziri Mkuu Mh.Mizengo Pinda, kuweka hadharani
Ripoti ya Tume ya
kuchunguza matokeo ya kidato cha nne iliyoundwa mwaka jana.
Akisoma tamko hilo mbele ya waandishi wa habari leo Jijini Dar es
Salaam, Mkurugenzi wa Mtandao wa wanafunzi nchini, Bw.Alphonce Lusako
amesema kuwa, wanamtaka Waziri Mkuu Pinda kutoa ripoti hadharani ndani ya wiki moja.
Aidha, Bw.Alphonse amebainisha kuwa pamoja na juhudi zinazofanywa na
Serikali kuimarisha elimu nchini, bado sekta ya elimu haijaboreshwa
inavyostahili.

0 Comments