Mhariri:Herman Kihwili.IMEWEKWA NOVEMBA 17.2013 SAA 02:46 USIKU
Cameroon imepata nafasi ya kushiriki katika Kombe la Dunia 2014 baada ya kuipatia kipigo kizito timu ya Tunisia kwa ushindi wa 4-1
katika uwanja wa Ahmadou Ahidjo mjini Yaounde.
katika uwanja wa Ahmadou Ahidjo mjini Yaounde.
Bao la kwanza la Cameroon liliwekwa nyavuni katika dakika 4 na Pierre Webo,wakati Benjamin Moukandjo akipachika bao la pili katika dakika ya 30, na mchezaji Jean Makoun akiipatia mabao mawili Cameroon katika dakika ya 66 na 86 .
katika mechi ya kwanza timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana,na sasa Cameroon imekuwa timu ya tatu ya Afrika kufuzu kwenda brazil baada ya Ivory Coast na Nigeria.
katika mechi ya kwanza timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana,na sasa Cameroon imekuwa timu ya tatu ya Afrika kufuzu kwenda brazil baada ya Ivory Coast na Nigeria.
![]() |
| Jean Makoun |
Bao pekee la kufutia machozi la Tunisia lilifungwa na Ahmed Akaichi katika dakika ya 51.
Cameroon: Itandje; Nkoulou, Chedjou, Mbia (Nounkeu
70’), Assou-Ekotto, Song, Makoun, Enoh, Moukandjo (Nguemo 83’), Webo
(Choupo-Moting 63’), Eto’o
Tunisia: Chrifia; Derbali, Mikari, Haggui, Benyoussef,
Ragued, Yahya (Allagui 74’), Chikhaoui (Camus 46’), Ben Youssef,
Chermiti (Akaichi 46’), Khalifa

0 Comments