Ticker

6/recent/ticker-posts

TENNIS & MBIO ZA MAGALI:Sebastian Vettel apata ushindi wa nne mfululizo,na katika tennis,licha ya kushindwa na Novak Djokovic, Rafael Nadal atangazwa mchezaji bora duniani huko China.

 IMEWEKWA OCTOBA 7,2013 SAA 06:26 USIKU
Sebastien Vettel
Timu ya magari ya Red Bull pamoja na dereva wake Sebastian Vettel wametoa mfano unaofaa kuigwa wa mchezo wa mbio za
magari kwa ustaadi wa dereva huyo na ubora wa gari kwenye mbio za Korea jumapili. 
Huu ukiwa ushindi wa mara nne mfululizo na wa nane msimu huu na mara 34 katika kipindi kifupi cha kushiriki mashindano.
Mpinzani wake wa karibu Fernando Alonso wa timu ya magari ya Ferrari aliweza tu kumaliza katika nafasi ya sita na hivyo kumfungulia Mjerumani fursa ya kutangazwa mshindi wa mashindano haya msimu huu wa 2013 kwenye mashindano yatakayofanyika nchini Japan jumapili ijayo.
Na kwenye mashindano ya mchezo wa Tennis ya Uchina au China open aliyekua mchezaji bora duniani Novak Djokovic alionyesha sababu ya kushikilia hadhi hio kwa mda mrefu kwa kumkandika mtani wake Rafael Nadal 6 -3, 6 -4 na hivyo kutoa ushindi wa Kombe la China.
Hata hivyo licha ya kushindwa Rafael Nadal atatangazwa mchezaji bora duniani bora kwa kuweza kufika fainali ya China.

CHANZO:BBC swahili

Post a Comment

0 Comments