Ticker

6/recent/ticker-posts

MSHABIKI WA TOTTENHAM WAPUUZA ONYO WALILOPEWA NA POLISI PAMOJA NA UONGOZI WA KLABU HIYO

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA OCTOBA 8,2013 SAA 09:16 USIKU
Mashabiki wa klabu ya Tottenham Hotspur wamekejeli amri ya polisi na klabu yao kwa kutotumia tamko "Yid" uwanjani na nje ya
uwanja,kwa kuendelea kulitumia katika mechi  yao  dhidi ya West Ham United.
Na wakati wakishangilia kwa neno hilo ambalo lilikuwa likitumiwa enzi za utawala wa kiimla wa hitler kuwaponza wayahudi,ni neno ambalo linachukuliwa kama matusi,mashabiki wa West Ham United walijibu kwa sauti za juu wakisema ni ubaguzi wa rangi.
Adolf Hitler
Haijulikani polisi itachukua hatua gani baada ya wiki nzima kuonya mashabiki kuwa yeyote atakaye patikana akilitumia neno hilo atakamatwa.
Mwezi uliopita, mwenyekiti wa chama cha mpira ', Clarke Carlisle, alisema mashabiki lazima wapigwe marufuku kwa kutumia neno hilo, lakini Waziri Mkuu David Cameron amesema watu hawapaswi kushitakiwa isipokuwa kama wakitumiwa kama tusi.


Post a Comment

0 Comments