Ticker

6/recent/ticker-posts

ARSENAL 1 BURUSSIA DORTMUND 2:LEWANDOWSKI ALETA BALAA TENA

 IMEWEKWA OKTOBA 23,2013 SAA 7:19 USIKU

Robert Lewandowski ameweza kuwafanya mashabiki wa Arsenal duniani kuwa wadogo baada ya kuipatia timu yake ya Dortmund
kumbukumbu nzuri ya  ushindi wa 2-1 katika ligi ya Mabingwa jana Jumanne usiku nakufanya kuongoza katika Kundi F katika mchezo huo uliopingwa katika uwanja wa kwenye Uwanja wa Emirates.
Kwenda mbele: Henrikh Mkhitaryan akifunga bao la kwanza kwa upande wa  Borussia Dortmund
Viongozi hao wa Ligi Kuu ya Barclays pamoja na kupambana kutoka nyuma lakini  katika dakika ya 16 Henrikh Mkhitaryan aliweza kuukwamisha mpira wavuni,kisha mchezaji wa Arsenal Olivier Giroud akaweza kuisawazishia timu yake katika dakika ya 41.
 Giroud akifunga bao la kwanza
Sare isiyokuwa na matumaini:Olivier Giroud  akishangilia baada ya kuisawazishia Arsenal na kufanya matokeo kuwa 1-1
Baada ya mapumziko Arsenal walionekana  kuzidi kulishambulia lango la Borussia Dortmund lakini Robert Lewandowski alipata nafasi katika dakika ya 82 nakuweza kuifungia Dortmund bao la pili na la ushindi.
Ushindi nje ya  nyumbani: Lewandowskiakifunga bao la ushindi

Pigo kuumia: Jack Wilshere akipatiwa matibabu baada ya kuumia
Wilshere akianngalia nusu ya pili na huku akiwekewa barafu juu ya kifundo cha mguu wake


Kikosi cha Arsenal: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Ramsey (Bendtner 86), Arteta, Wilshere (Cazorla 58), Ozil, Rosicky (Gnabry 89), Giroud.

Akiba wasiutumika: Fabianski, Vermaelen, Monreal, Jenkinson
Kadi za njano: Rosicky, Ozil.
Mfungaji: Giroud 41.
Kikosi cha Borussia Dortmund: Weidenfeller, Grosskreutz, Subotic, Hummels, Schmelzer, Bender, Sahin, Blaszczykowski (Aubameyang 67), Mkhitaryan (Hofmann 66), Reus (Papastathopoulos 87), Lewandowski.
Akiba wasiotumika: Langerak, Kirch, Schieber, Durm.
Kadi za njano: Hummels,Lewandowski, Bender.
Wafungaji: Mkhitaryan 16, Lewandowski 82.
Walioudhulia: 59,000
Refa: Jonas Eriksson (Sweden)

 



Post a Comment

0 Comments