IMEWEKWA SEPT 11,2013 SAA 11:50 JIONI
Thomas Bach ameongeza ushindi mwingine baada ya ule wa medali ya dhahabu
katika mchezo wa fencing katika olimpiki ya mwaka 1971 wakati
alipochaguliwa kuwa rais wa tisa wa kamati ya olimpiki ya kimataifa IOC.
![]() |
| Thomas Bach |
Bach mwenye umri wa miaka 59 raia wa Ujerumani na ambaye pia ni
mwanasheria amesherehekea ushindi wake wa kishindo dhidi ya wagombea
wengine watano katika duru ya pili ya uchaguzi katika
uchaguzi uliokuwa
wa siri wa kamati hiyo ya IOC katika kikao cha 125 leo
Jumanne(10.09.2013).![]() |
| Thomas Bach akitangazwa rasmi kuwa mshindi |
Bach ambaye ni mtu mwenye hamasa kubwa ya kiutendaji alikuwa mtu ambaye
anapigiwa upatu kuchukua nafasi ya Jacques Rogge kwa muda mrefu na sasa
amenyakua wadhifa huo wa juu katika spoti duniani miaka 22 baada ya
kuchaguliwa kuingia katika kamati hiyo ya IOC.
Kumbukumbu
"Uff!" amesema , katika matamshi yake ya kwanza kama rais wa IOC. "Hii
ni ishara kubwa kabisa ya kuonesha imani kwangu na kuniamini.
"Wacha tuwe pamoja katika kundi hili la muziki wa pamoja, tucheze muziki
kwa pamoja kwa ajili ya hali bora ya baadaye," ameahidi Bach.
![]() |
| Thomas Bach katika michezo ya olimpiki mwaka 1972 |
Bach anakumbuka siku zake za kucheza mchezo wa fencing ambazo pia
zilimfanya kunyakua ubingwa wa dunia mwaka 1977 mjini Buenos Aires, na
aliwashukuru wale ambao hawakumpigia kura na wale waliompigia kura.
"Pia nitafanyakazi kwa ajili yenu na pamoja na nyie katika miaka ijayo
na nataka mniamini pia," amesema. Mlango wangu utakuwa wazi, masikio
yangu na moyo wangu kila wakati vitakuwa wazi."
Rogge ambaye anaondoka amesema katika ufunguzi wa kikao hicho mjini
Buenos Aires kuwa "rais mpya atakuwa na wakati mzuri sana katika maisha
yake."
Changamoto
Rogge anafahamu kutokana na miaka 12 ya uongozi wake, pia kuwa kuna
changamoto mbele ya Bach, ambaye amechaguliwa hadi mwaka 2021 na kisha
anaweza kuomba uongozi kwa kipindi cha pili na cha mwisho , cha miaka
minne.
Changamoto hizo ni pamoja na michezo ijayo ya majira ya baridi mjini
Sochi mwaka 2014, huku kukiwa na wasi wasi wa usalama kuhusiana na
vitisho vya kigaidi pamoja na utata kuhusiana na upinzani kuhusu
mashoga, pamoja na michezo ya mjini Rio mwaka 2016 ambayo imekumbwa na
uchelewesho wa ujunzi.
![]() |
| Alama ya Olimpiki |
Mageuzi ya wakati wote ya mipango wa michezo ya olimpiki na olimpiki kwa
vijana , kuendeleza utajiri mkubwa wa kamati ya IOC katika nyakati
ngumu za kiuchumi, na kuhakikisha maadili ya olimpiki dhidi ya matumizi
ya madawa ya kuongeza nguvu pamoja na kupanga matokeo ni majukumu ambayo
yanamsubiri Bach.
Bach alitangaza kuwania wadhifa huo Mei 9 akifanya kampeni iliyopewa
jina la "Umoja katika hali anuai," lakini alikuwa akiifanya kazi kupanda
juu ili kufikia lengo lake la kuwa kileleni mwa kamati ya kimataifa ya
olimpiki kwa miaka kadha.
Amekuwa makamu wa rais wa OIC kwa miaka kumi chini ya Rogge,
akifanyakazi katika tume 14 na alitumia miaka 15 katika bodi yenye
ushawishi mkubwa wa utendaji ambayo inatoa maamuzi, alikuwa mwenyekiti
wa tume ya sheria na kamati ya nidhamu katika michezo.
![]() |
| Thomas Bach akihutubia kikao cha OIC |
Uzoefu wake huu mkubwa na mtandao umemruhusu kufahamu mambo mbali mbali
ya matokeo mazuri katika michezo duniani hali ambayo imemfanya kuwa ,
"chaguo lisilo kuwa na shaka," kwa mujibu wa mjumbe mmoja wa heshima wa
IOC Walter Troeger..





0 Comments